• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, December 18, 2012

    MUONGOZAJI WA FILAMU ZA KIBONGO ASAKWA NA POLISI KWA ‘KUMBAKA’ MSANII CHIPUKIZI


    MUONGOZAJI na mtayarishaji wa filamu za Kibongo, Selles Mapunda “Director of Directors” (Pichani) anatafutwa na Polisi baada ya kushutumiwa kumbaka msanii chipukizi Nancy Njozi maeneo ya Mwananyamala.
    Kwa mujibu wa tovuti ya filamu central, Binti huyo baada ya tukio hilo alikwenda kituo kidogo cha Polisi CCM Mwinyijuma na kupewa RB MWJ/RB/8361/2012 TUHUMA KUBAKA, baadae kesi ikahamishiwa kituo kikubwa cha Polisi Osterbay na kupewa taarifa OB/RB/2012 na OB/IR/11918/2012 KUBAKA.
    Picha ilikuwa hivi: Mapunda aliaandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook HELLO! BAADA YA KUKAMILIKA KWA FILAMU YA “THE RETURN OF J-LO” SELLES BUSINESS INC. INAANDAA FILAMU MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA “CROSS OF LOVE” FILAMU ITASHIRIKISHA WASANII NGULI HAPA NCHINI KAMA WEMA SEPETU, DIVA E.T.C PIA KUNA NAFASI ZA WASANII WACHANGA 15.

    USAHILI UTAFANYIKA TAREHE 14-11-2012 KATIKA VIWANJ VYA LEADERS CLUB SAA 4 ASUBUHI, FOMU ZA KUOMBA KUJIUNGA ZINAPATIKANA SINZA PALESTINA (AL-JAZEERA ENTERTAINMENT), DEMONTE WINE SHOP, MWANANYAMALA (KWA AUNTY EZEKIEL) NA UHURU PEAK, KINONDONI AU PIGA SIMU NO; 0714 868 999 AU 0655212720
(FOMU ZINAANZA KUTOLEWA KESHO JUMATANO SAA 4 ASUBUHI.
.
    “Nilipoona ujumbe huu nilimpigia simu kwa ajili ya kutaka kushiriki katika usahili, alipokea baadae alinipigia na kuniambia kuwa nafasi ni chache kwa hiyo nifike Mwanyamala kwa ajili ya kufanyiwa usahili, nilifika na kumkuta sehemu aliyonielezea na kunipeleka Mwananyamala ndani ndani na hatimaye kunibaka,”anasema Nancy.
    Baada ya kuongea na mhusika Filamu Central ilimtafuta Selles lakini hakuna hata simu yake mmoja ilikuwa ikipatikana, baada ya kushindikana tumtafuta rafiki wa karibu na Mapunda, Kambarage.
    Filamu Central inaandika kuwa Kambarage alikiri kwa kusema kuwa habari hizo amezisikia lakini anachofahamu ni kuwa zimetengenezwa na msichana ambaye ni mpenzi wa Mapunda ili kumharibia baada ya kuomba pesa na kunyimwa.
    Filamu Central bado inamtafuta Mapunda ili kubaini ukweli halisi kwani hata ofisini kwake hapatikani kwa sasa jambo lilnalozua utata.Sorce DTV TAGZWEEKLY.

    No comments:

    3500K