• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, December 20, 2012

    KAULI YA DIAMONDI JUU YA KUVUJA KWA VIDEO YAKE MPYA-'KESHO'


    na dj sek blog

    Party baada ya wazazi kumkubai mchumba wa Diamond 
    Bata 
    She is hot au sio?












    Diamond Platnumz amesema kuwa video yake mpya ya ‘Kesho’ iliyofanyika nchini Kenya imetoka mtandaoni kimakosa.

    Akiongea na kipindi cha Power Jams leo, Diamond amesema Ogopa Djs waliofanya video hiyo waliiupload kwenye mtandao wa Youtube ili wamtumie link Diamond na uongozi wake waione kama iko sawa ili wakabidhiwe.

    Amesema aligundua kuwa kuna kosa katika title ya producer ambayo imeandikwa ‘Wasafi Entertainment’ badala ya Marco Chali na akawataka wabadilishe. Hata hivyo Ogopa walisema wasingeweza kuitoa hiyo ya kwenye Youtube kwa kudai kuwa wangepoteza viewers ila watabadilisha version ya kusambaza kwenye TV.

    Hata hivyo Diamond hakukubaliana na wazo hilo na kusisitiza kuwa waiondoe kwanza kwenye mtandao na ndipo Ogopa waliitoa japo walikuwa wameshachelewa kwakuwa kuna watu walikuwa wameidownload tayari na kuiupload kwenye akaunti zao.

    Amesema video yenyewe itatoka rasmi Ijumaa hii na bado yeye na uongozi wake wapo kwenye mazungumzo ya iwapo audio yake itoke sasa ama baadaye.

    Na hizi ndio screen shots 20 bora za video hiyo

    No comments:

    3500K