• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, August 23, 2012

    Bila Million 10 Siwezi Cheza Movie ya Mtu" Rose Ndauka


    Rose Ndauka

    Msanii Rose Ndauka ni mmoja kati nyota wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo, ambapo amedai kuwa baada ya kushiriki kwenye filamu nyingi na kuonesha uwezo wake sasa kama kuna mtu anayehitaji kumtumia ndani ya kazi yake basi lazima awe na shilingi milioni 10 keshi mbali na hapa itakuwa ngumu kushiriki.

    Kiwango cha fedha cha msanii huyo ineosha kuwa anajua thamani yake kama msanii mkubwa anayehitaji kuwa lulu ndani ya tasnia hiyo. Baadhi ya filamu alizowahi kung’arisha mwanadada huyu ni pamoja na ‘Because of You’, ‘Love Me Or Love Me Not’ na nyingine nyingi.


    Akiongea na mwandishi wa mtandao wa DarTalk aliyetaka kujua kama Rose anatambua thamani yake, ambapo alidai kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuficha na kuendelea kuumia, na ndiyo maana ameamua kuweka wazi ishu hiyo kuwa hachezi filamu ya mtu bila muafaka wa kiwango cha fedha alichokitaja.

    “Inatakiwa tufikie kipindi wasanii tujue thamani yetu kwani wapo baadhi ya wasanii wengine wana majina makubwa lakini wanafanya filamu kwa bei za chini, lakini siwezi kulaumu kwani kila mtu anafanya kwa mipango yake,” alidai.

    No comments:

    3500K