• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, June 13, 2012

    WAKILISHI WA TANZANIA MISS WORLD TANZANIA KUTAFUTWA JUMAMOSI JUNI 16

    Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kudhamini shindano la kumpata mrembo atakewakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu, yanayojulikana kama “Miss World 2012.
    Akizungumzia Udhamini wa shindano hilo linalojulikana kama “Redd’s Miss World 2012” Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa mashindano ya urembo hapa nchini Bw. Hashim Lundenga alisema; Ninajua wadau wengi wa tasnia ya urembo watastuka kuona mabadiliko haya, hii inatokana na kubadilika kwa ratiba ya mashindano ya Miss World toka mwezi wa December ilivyokuwa ikifanyika awali na sasa yatakuwa yakifanyika mwezi Julai hivyo kuwa na tofauti kubwa na ratiba ya mashindano yetu ya Redds Miss Tanzania ambayo huanza mwezi Mei na kumalizika Septemba. Ili tusipoteze nafasi yetu ya kushiriki mwaka huu, kamati ya Miss Tanzania kwa ridhaa ya Serikali, iliamua kufanya shindano dogo “Mini competition” ambalo litatupatia mshindi atakae wakilisha Taifa katika mshindano hayo makubwa Duniani.  Warembo 10 wataingia kambini tarehe 13 hadi tarehe 17 June, na shindano litafanyika siku ya Juma Mosi tarehe 16 June katika ukumbi mpya wenye hadhi ya kimataifa wa 327 Club, uliopo Mikocheni. Mshindi atazawadiwa pesa taslim shilingi Milioni mbili, na kupatiwa maandalizi yote kwa ajili ya matayarisho ya safari yake kwenda kwenye mashindano ya Miss World 2012 yatakayofanyika Inner Mongolia – China. Kutokana na umuhimu wa kufanya shindano hili tuliwaomba wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, kinywaji cha Redds ili watuwezeshe kufanikisha mchakato huu, nao bila kusita wakakubali. Hivyo tunawapongeza sana Redds kwa mchango wao mkubwa katika tasnia ya Urembo hapa nchini.

    No comments:

    3500K