• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, June 13, 2012

    MAJAMBAZI WAWILI WANASAKWA KWA KUWAPORA RAIA WA UHOLANZI

     
    Na. mwandishi wangu kutoka, Dodoma
     
     Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawasaka Watu wawili kwa tuhuma za  Unyang’anyi wa kutumia nguvu baada ya kuwatisha kwa  jambia wasichana wawili raia wa Uholanzi  na kisha  kuwapora vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni moja laki mbili na sitini na nne elfu.
     
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo lilitokea muda wa saa saba na dakika arobaini na tano mchana katika  eneo la area D Wilaya ya Dodoma Mjini,  Karibu na nyumba inayojengwa kwa ajili ya 0fisi na  Makazi ya Mh. Waziri  Mkuu  Bw. MIZENGO KAYANDA  PETER PINDA.
    Alitaja vitu vilivyoporwa katiika tukio hilo kuwa ni Kamera ya digitali aina ya Canon, Simu mbili za mkononi aina ya Nokia na Samsung, Begi la Mgongoni, Viatu vya wazi pea mbili (Sandal) Taulo la Hostel, Sketi, Wallet na Pesa za kitanzania shilingi 40,000/=.
    Aidha aliwataja Waathirika  wa Unyang’anyi huo kuwa ni wa LISA D/O LEMEN mwenye umri wa miaka (19) na FLEUR D/O EDITH SCHOLTEN Mwenye Umri wa miaka (17) wote ni Raia wa Uholanzi ambao wako nchini kama  waalimu  wa shule ya msingi na sekondari ya Saint Germa iliyoko jijini Arusha inayofundisha watoto  ambao wazazi wao wamefungwa gerezani.
    “Raia hao wa Uholanzi ambao walikuja kutembea Mjini Dodoma wakitokea Arusha walifikia katika Hostel ya Saint Maria ambayo wanaishi wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule za kutwa   za mjini Dodoma”:

    Kamanda ZELOTHE STEPHEN alisema kuwa wageni hao walioporwa  vitu  hivyo, baada ya kufika katika eneo hilo wakiwa na mwenyeji wao aliyejulikana kwa jina la Sister PONSIAN PROTAS MATAKA miaka (43) ambaye anaishi katika Hostel waliyofikia wageni hao ya Saint Maria ilyopo eneo la Uhindini.

    No comments:

    3500K