K
|
amati
ya Uchaguzi ya TFF inawataarifu wadau na wapenzi wa soka kuwa mchakato wa
uchaguzi wa viongozi wa YANGA kujaza nafasi zilizowazi za Kamati ya Utendaji
unaendelea vizuri chini ya Kamati ya Uchaguzi ya YANGA.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepokea
kutoka Kamati ya Uchaguzi ya YANGA nakala za fomu za maombi ya uongozi wa YANGA
pamoja na nakala za vyeti vya elimu vya waombaji uongozi kama
sehemu ya taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi huo wa YANGA. Kamati ya
Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa baadhi ya waombaji uongozi wamewasilisha nakala
za vyeti vya kuhudhuria masomo ya sekondari (Secondary School Leaving
Certificate) badala ya nakala za vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya
sekondari (Certificate of Secondary Education).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekwisha
ielekeza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kuwataka wagombea wote kuzingatia Kanuni
za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(4) na (5) inayowataka wagombea wote
kujaza Fomu Na.1 ya maombi ya uongozi na kuambatanisha nakala ya cheti cha
Elimu ya Sekondari (Certificate of Secondary Education) kama ilivyoainishwa kwenye Fomu Na.1 kipengere Na.9.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya YANGA iwashauri
wagombea ambao vyeti vyao vimepotea wawasiliane na Baraza la Mitihani la
Tanzania (NECTA) kwa maandishi ili kupata ‘Statement of Examination Results’
itakayotumwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya YANGA kupitia TFF kuthibitisha kuwa
wamehitimu elimu ya kidato cha nne.
Uhakiki wa vyeti vya elimu ya
sekondari vya waombaji uongozi hufanywa na NECTA na vyuo husika kwa elimu ya
juu kwa chaguzi za wanachama wa TFF. Wanachama wote wa TFF wanatakiwa
kuzingatia kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment