Imeelezwa kuwa zaidi ya watu 600
waliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia
sheria mkononi katika kipindi cha mwaka jana pekee.
Hayo
yamesemwa na Wakili na Afisa wa ufuatiliaji wa Haki za Binadamu kutoka katika kituo
cha Haki za Binadamu (LHRC), Laetitia Ntagazwa wakati akitoa mada kwenye
mafunzo ya waangalizi wa Haki za Binadamu wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
yaliyofanyika Jijini Mbeya.
Amesema
utafiti uliofanywa na LHRC umeonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka jana pekee
watu zaidi ya 600 wameuawa kwa kupigwa na wananchi, hali ambayo inaashiria kuwa
vitendo vya watu kujichukulia sheria mkononi vinazidi kukithiri nchini.
Aidha,
Ntagazwa amesema kufuatia kuongezeka kwa vitendo hivyo ambavyo ni kinyume
cha sheria za nchi na ukiukwaji wa haki za Binadamu, Kituo cha Haki za Binadamu
kimeamua kuchukua hatua ya kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa elimu kwa
wananchi juu ya athari za kujichukulia sheria mkononi.
Amesema
miongoni mwa mambo ambayo LHRC kinataka kushirikiana kwa karibu na Jeshi la
Polisi ni kampeni ya utii bila Shuruti, ambapo wameamua kuwashirikisha Polisi
kila mahali wanapokwenda kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waangalizi wa haki
za binadamu.
Imeandikwa na Angella Sulluci, Mbeya
No comments:
Post a Comment