• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, June 26, 2012

    Ommy D afungukia ishu ya kujiunga Freemason



    NI wiki ya Ommy Dimpoz, mwanamuziki ambaye jina lake kamili ni Omary Faraji Nyembo. Naye anajibu na kufafanua juu ya yale ambayo mlimuuliza.
    Matarajio yake
    Dimpoz wewe ni msanii mahiri kunako gemu la muziki, vipi matarajio yako? Salim Liundi, Dar, 0658110395
    OMMY DIMPOZ: Matarajio yangu ni kufika mbali zaidi kwa kujitangaza kimataifa.
    Yeye na Irene Uwoya
    Ommy Dimpoz eti uliwahi kutoka kimapenzi na Irene Uwoya? Msomaji, Dar.
    OMMY DIMPOZ: Siyo kweli.
    Eti anakopi mashairi
    Kiukweli Ommy unatisha sana, epukana na skendo zitakuharibia jina, kuna baadhi ya watu wanasema unakopi mashairi, je ni kweli? 0715433234
    OMMY DIMPOZ: Siyo kweli, mimi nafanya kazi zangu mwenyewe sikopi.
    Hongera
    Umeingia kwenye gemu vizuri, watu wamekukubali hongera. Cassian, Iringa, 0655202202
    OMMY DIMPOZ: Asante.
    Kuhusu yeye
    Ommy Dimpoz wewe ni kabila gani, umezaliwa wapi, una miaka mingapi? Ramadhani Khamisi, Tanga, 0717236195
    OMMY DIMPOZ: Mimi ni Mmanyema, nimezaliwa hapa Dar, nina miaka 25.
    Kumuacha Sara?
    Big up Ommy, vipi kuhusu Sara mpenzi wako nasikia umemuacha baada ya kupata umaarufu? Msomaji, 0718021155
    OMMY DIMPOZ: Hapana siyo kweli, mimi siko katika uhusiano na mtu yeyote.
    Kuhusu mke
    Ommy unadai kuwa huna mke wala mchumba, je ni lini utakuwa na mke? James Lucas, Dar, 0657800439
    OMMY DIMPOZ: Kwa sasa naangalia kwanza maisha muda ukifika naamini Mungu atanipa mke mwema.
    Kujiunga Freemason
    Kaka Ommy nakukubali uko juu, je ni kweli una mpango wa kujiunga na Freemason? Michael Stephano, Tanga, 0713152125
    OMMY DIMPOZ: Hapana sina mpango huo.
    Hili la dimpoz, mh!
    Ommy una kipaji na nyimbo zako ni nzuri ila uache kujinadi na dimpoz mbona hata mimi ninazo? Msomaji, 0654903166
    OMMY DIMPOZ: Sawa nimesikia ushauri wako.
    Yeye handsome?
    Nakukubali sana kwa kazi zako lakini kwa nini unajiita super handsome? Julius Myinga, Iringa, 0717162049
    OMMY DIMPOZ: Muziki siku zote unahitaji vitu vya ziada kwa hiyo najiita tu siyo kweli hivyo ni vionjo tu.
    Huyu anamjua
    Mimi nakufahamu kwa jila la Omary Faraji, umemaliza kidato cha nne 2008 Mbezi High School, ulikuwa unapenda kuimba tangu shuleni. Aziza Omary, Dar, 0778704805
    OMMY DIMPOZ: Kweli kabisa.
    Faida aliyopata
    Toka uwe staa ni mambo gani ya faida umepata? Elia, Iringa, 0718085308
    OMMY DIMPOZ: Faida kubwa nimejuana na watu wengi, naweza kujikimu kimaisha.
    Staili yake ya nywele ni poa
    Ommy hiyo staili ya nywele inakutoa kinoma? Amy, Dar, 0717204990
    OMMY DIMPOZ: Nashukuru sana.
    Historia yake
    Ningependa kujua historia yako kwa ufupi. Zawadi, Iringa, 0712147586
    OMMY DIMPOZ: Nimezaliwa mwaka 1987 hapa jijini Dar, nimesomea Business Administration Chuo cha IFM ngazi ya Cheti, muziki nilianza miaka 6 iliyopita.
    Yeye na Agatha
    Mimi ni shabiki wako napenda sana jinsi unavyojimwaga stejini, nilisikia unatoka kimapenzi na Agatha, ni kweli? Janeth, 0764474546
    OMMY DIMPOZ: Hapana na sijawahi kuwa na mpenzi mwenye jina hilo.
    Kuhusu kukopi wimbo wa Baadae
    Ommy Dimpoz mbona wimbo wako wa ‘Baadae’ umemuiga Michael Jackson kuna wimbo ameimba kama huo na kama unabisha nipigie. Deo, Dar, 0752961087
    OMMY DIMPOZ: Kama una ushahidi kuwa mimi nimekopi wimbo naomba uupeleke Global.
    Huyu anaomba uchumba
    Nakupenda sana Ommy Dimpoz na ningependa uwe mchumba wangu. Rose Claudio, Mwanza, 0762054812
    OMMY DIMPOZ: Nakupenda sana lakini kwa sasa siko tayari kuwa na mchumba.
    Pongezi
    Nakupongeza Ommy Dimpoz kwa kazi nzuri za Nainai na Baadae, je vipi kuhusu lile sakata lako na Cyrill? Hamis Mkumba, Kibaha, 0719612680
    OMMY DIMPOZ: Nashukuru kwa pongezi.
    Usumbufu wa mademu
    Kuwa makini na kina dada wa mjini maana unavyodatisha nahisi unasumbuliwa sana. Hellen, Dar, 0718210444
    OMMY DIMPOZ: Kweli lakini niko makini sana.
    Asili ya jina la Ommy Dimpoz
    Kaka Ommy naomba kujua asili ya jina la Ommy Dimpoz. Eliza Masunga, Mwanza, 0718415622
    OMMY DIMPOZ: Kweli limetokana na mashavu yangu kubonyea na mashabiki ndiyo walinipa hilo jina.
    Anamkubali Chris Brown
    Big up kwa kazi nzuri, ningependa kujua ni msanii gani ambaye unamkubali mamtoni? Said Gonza, Zanzibar, 0773356360
    OMMY DIMPOZ: Kwa sasa wapo wasanii wengi sana wanafanya vizuri lakini mimi nampenda sana Criss

    No comments:

    3500K