Pichani ni Dokta Steven Ulimboka kama anavyoonekana baada ya kuokotwa
leo maeneo ya Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam huko Tegeta
alikotupwa na watu wasiojulikana baada ya kumteka jana usiku akiwa
nyumbani kwake. Kwa maelezo yake mwenyewe alisema kuwa akiwa nyumbani
kwake
jana usiku walikuja watu waliodai kuwa wao ni askari
ambao walimchukua na kumpakia kwenye gari ndigi isiyo na plate namba na
kisha waliekea barabara ya Bagamoyo ambako baadae walimfunga kitammbaa
usoni na kuanza kumpiga sana huku wakidai kuwa kama wangekuwa na sindano
ya sumu wangemchoma afe kwani amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu, Kisha
baada ya muda walimtupa Dokta akiwa hajitambui mpaka alipookotwa leo na
sasa yuko Muhimbili kwa matibabu!!Wednesday, June 27, 2012
Home
Unlabelled
MGOMO WA MADAKTARI: DR. ULIMBOKA ATEKWA,KUPIGWA NA KUJERUHIWA VIBAYA SANA!!
No comments:
Post a Comment