• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Sunday, June 17, 2012

    LISA NDIYE MISS TANZANIA 2012



    Lisa katikati akiwa na wenzake

    KIMWANA Lisa Jensen usiku huu ameibuka kinara katika shindano maalum la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katka shindano la Miss World mwaka huu, lililofanyika kwenye ukumbi wa 327, Mikocheni, Dar es Salaam.
    Shindano hilo, lililoshirikisha washiriki wa zamani wa Miss Tanzania ambao hawajawahi kushinda, dalili za Lisa kushinda zilionekana tangu mwanzo, kutokana na kuwafunika washiriki ‘ile mbayaaa’ washiriki wenzake tisa.
    Shindano hilo, lilianzia kwa warembo kucheza shoo ya ufunguzi kama ilivyo ada ya mashindano ya Miss Tanzania, baadaye wakapita na vazi la ubunifu, ufukweni na kumalizia na vazi la jioni, ambako kote Miss Mara wa 2006 alifunika mbaya.
    Aliyemfuatia Lisa ni Hamisa Hassan kutoka Kinondoni, wakati mshindi wa tatu alikuwa ni Pendo Laiser Miss Arusha 2008 na wengine walioingia tano bora ni Stella Mbuge na Jennifer Kakolaki.
    Washiriki wengine ni Glorybayanca Mayowa, Queen Issa, Christine William, Mwajabu Juma na Neema Saleh.
    Shindano hili, linafanyika kufuatia kalenda ya mashindano ya Miss Tanzania kubadilika na washindi wa mashindano ya mwaka huu ngazi ya awali watashiriki katika shindano la Miss Tanzania baadaye mwaka huu, kumpata mwakilishi wa Miss World mwakani.
    Waalikwa wakifuatilia shindano

    Warembo shoo ya ufunguzi

    Lisa akipongezwa na Salha, Miss Tanzania 2011 baada ya kuvikwa taji

    Lissa akipunga mkono katikati

    Majaji wakipiga hesabu

    Jaji Mkuu wakitangaza top 5

    Majaji kazini

    Waalikwa

    Waalikwa
    Majaji
    Jane John na kaka ake BIN ZUBEIRY
    Fimbo Butallah na kimwana
    JK akisomesha
    Sura za furaha
    Glory na rafiki zake
    Hizi kazi zetu hizi, we acha tu. Issa Mnally 'Duwa Chee'
    Prashant anatetwa mbele yake
    Waalikwa
    Top three
    Wataalamu
    Top 5
    Salha anamvalisha taji Lissa
    Mwaaa! hongera mama, Salha akimvisha taji Lissa
    Waalikwa, Juma Pinto kushoto, Benny Kisaka na Jackson Kalikumtima
    You might also like:

    No comments:

    3500K