KATIKA hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo movie wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa Baba mzazi wa msanii mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea kwa uzuni amesema kuwa hata wale waliofika jana katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji bali walifika kwa ajili ya kumsanifu.
FC ilifanya utafiti ili kubaini hilo kwa kuwapigia simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita kwa masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa
kusema kuwa ni kweli uongozi wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya msanii huyo kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema bwana huwa hashiriki katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo na Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema anabagua kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga alipigiwa simu ili ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location, hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya wenzake.
Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya mtangazaji wa kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakini hawakuwa na dhamira ya kweli mioyoni mwao.
No comments:
Post a Comment