WANAUME wawili wamefariki dunia kwa
kuchomwa visu na kupigwa na mawe katika tukio la kugombea mwanamke wilayani
Tarime, Mara.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, Justus Kamugisha, alisema tukio
hilo limetokea juzi kwenye eneo la gulio katika Kijiji cha Nyibaso, Tarafa ya
Ingwe, wilayani Tarime.
Alisema
chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, ambapo wanaume hao walikuwa
wakigombania mwanamke huyo ambaye ni mjane.
Alisema
katika tukio hilo, mwanamume aliyefahamika kwa jina moja la Nyamureba, mkazi wa
Kijiji cha Matanka, wilayani Serengeti, alimshambulia Juma Mseti au Marwa (20),
mkazi wa Kijiji cha Nyibaso kwa kumchoma na visu tumboni na kusababisha kifo
chake papo hapo.
Alisema
baada ya kumuua mwenzake, mwanamume huyo alikimbia, ambapo wananchi wakiongozwa
na ndugu wa marehemu, walimfukuza na kufanikiwa kumkamata na kumchoma visu na
kumpiga kwa mawe hadi kumuua.
Alisema
kuwa mwanamke aliyekuwa anagombaniwa na wanaume hao ametoroka.
CHANZO: Ahmed Makongo, TARIME
No comments:
Post a Comment