*Mwanamume mmoja anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mwenzake kwa
kumkata panga na kumchoma na kisu, baada ya kumwaga pombe yake.*
Kamanda Kamugisha alisema jana kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa
12:45 jioni katika Kitongoji cha Itandura, Kijiji cha Nyakunguru, wilayani
Tarime.
Alimtaja mwanamume anayetafutwa na polisi kuwa ni Makuri Mcharo, mkazi wa
kikijiji hicho na kwamba anatuhumiwa kumuua Makuri Hamisi (32) ambaye pia
ni mkazi wa kijiji hicho.
*CHANZO: Ahmed Makongo, TARIME*
No comments:
Post a Comment