CHANZO::JAIZMELALEO
Rais
wa Marekani Barack Obama amekula kiapo kwa ajili ya muhula wake wa pili jana,
katika hafla ambayo ilihudhuriwa na wanafamilia na waandishi wa habari tu.
Obama anaanza muhula wa pili
akikabiliwa na matatizo kadhaa nyumbani na nje, yakiwemo mgawanyiko mkubwa
mjini Washington kuhusu masuala mbalimbali, mpango wa Iran wa nyuklia, na
wapiganaji wa Kiislamu katika kanda ya Afrika ya kaskazini. Mapema jana, makamu
wa raia Joe Biden aliapishwa katika makaazi yake rasmi. Sherehe kubwa
inatarajiwa kufanyika leo katika jengo la Capitol mjini Washington. Hotuba ya
Obama inatarajiwa kujikita katika haja ya kufanya tahfif za kisiasa na
warepublican pale inapowezekana.
No comments:
Post a Comment