VIDEO inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford akijifungua imezua kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana kuichukua bila ridhaa ya mhusika na kuisambaza kwa watu mbalimbali.
“Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa anahaha kumjua aliyeisambaza lakini pia anahakikisha haiwafikiii watu wengine na vyombo vya habari kwani inamuonesha hatua kwa hatua akijifungua,” kilisema chanzo hicho
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Shamsa ambaye alisema: “Kiukweli nimeumia sana, hiyo video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu, kwa nini mtu aichukue na kuisambaza bila ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”
---------------- Mtandao huu haujafanikiwa kuipata video hiyo...
No comments:
Post a Comment