MUONGOZAJI
na mtayarishaji wa filamu za Kibongo, Selles Mapunda “Director of
Directors” (Pichani) anatafutwa na Polisi baada ya kushutumiwa kumbaka
msanii chipukizi Nancy Njozi maeneo ya Mwananyamala.
Kwa
mujibu wa tovuti ya filamu central, Binti huyo baada ya tukio hilo
alikwenda kituo kidogo cha Polisi CCM Mwinyijuma na kupewa RB
MWJ/RB/8361/2012 TUHUMA KUBAKA, baadae kesi ikahamishiwa kituo kikubwa
cha Polisi Osterbay na kupewa taarifa OB/RB/2012 na OB/IR/11918/2012
KUBAKA.
Picha
ilikuwa hivi: Mapunda aliaandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa
Facebook HELLO! BAADA YA KUKAMILIKA KWA FILAMU YA “THE RETURN OF J-LO”
SELLES BUSINESS INC. INAANDAA FILAMU MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA “CROSS
OF LOVE” FILAMU ITASHIRIKISHA WASANII NGULI HAPA NCHINI KAMA WEMA
SEPETU, DIVA E.T.C PIA KUNA NAFASI ZA WASANII WACHANGA 15.
USAHILI
UTAFANYIKA TAREHE 14-11-2012 KATIKA VIWANJ VYA LEADERS CLUB SAA 4
ASUBUHI, FOMU ZA KUOMBA KUJIUNGA ZINAPATIKANA SINZA PALESTINA
(AL-JAZEERA ENTERTAINMENT), DEMONTE WINE SHOP, MWANANYAMALA (KWA AUNTY
EZEKIEL) NA UHURU PEAK, KINONDONI AU PIGA SIMU NO; 0714 868 999 AU
0655212720
(FOMU ZINAANZA KUTOLEWA KESHO JUMATANO SAA 4 ASUBUHI.
.
“Nilipoona
ujumbe huu nilimpigia simu kwa ajili ya kutaka kushiriki katika
usahili, alipokea baadae alinipigia na kuniambia kuwa nafasi ni chache
kwa hiyo nifike Mwanyamala kwa ajili ya kufanyiwa usahili, nilifika na
kumkuta sehemu aliyonielezea na kunipeleka Mwananyamala ndani ndani na
hatimaye kunibaka,”anasema Nancy.
Baada
ya kuongea na mhusika Filamu Central ilimtafuta Selles lakini hakuna
hata simu yake mmoja ilikuwa ikipatikana, baada ya kushindikana
tumtafuta rafiki wa karibu na Mapunda, Kambarage.
Filamu Central inaandika kuwa Kambarage alikiri
kwa kusema kuwa habari hizo amezisikia lakini anachofahamu ni kuwa
zimetengenezwa na msichana ambaye ni mpenzi wa Mapunda ili kumharibia
baada ya kuomba pesa na kunyimwa.
Filamu
Central bado inamtafuta Mapunda ili kubaini ukweli halisi kwani hata
ofisini kwake hapatikani kwa sasa jambo lilnalozua utata.Sorce DTV
TAGZWEEKLY.
No comments:
Post a Comment