Dah!
kiukweli nimesikitishwa sana na tarifa hizi....mwanzoni nilipoanza
kupokea msg na simu toka kwa watu mbalimbali nikajua labda ni kamchezo
tu watu wameshaanza kuzusha kama kawaida yao dah! kumbe nikweli ndugu
yetu ametutangulia mbele ya haki... akizungumza na Clouds Media RPC mkoa
wa tanga alithibitisha kwa kusema kua Sharo Milionea alipata ajali leo
majira ya saa mbili usiku maeneo ya Maguzuni songa karibu na wilaya ya
Muheza akiwa anaelekea tanga kumuona Mama yake na gari aina ya Toyota
Harrier yenye namba za usajili T478 BVR.. aliendelea kusema kuwa gari
hiyo ilitoka nje ya barabara na kupinduka na kusababisha kifo cha msanii
huyo papohapo...aliiambia clouds media kuwa taarifa zaidi hazikuweza
kupatikana kwakua msanii huyo alikuwa yuko pekeyake kwenye gari.. na
kumalizia kuwa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Teule
wilayani Muheza.... |
No comments:
Post a Comment