NEWZ>>>FILEX MMARI
Tukio hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake lilichukua nafasi juzi Jumamosi, katika Ukumbi wa The Atriums Hotel, Sinza – Afrika Sana, Dar na kuhudhuriwa na ndugu wa pande zote mbili.
Kinyume na ilivyozoeleka, zoezi la kutoa mahari kufanyika nyumbani, kwa wawili hawa ilikuwa tofauti kwani kila kitu kilimalizikia ukumbini humo.
“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha tukio hili, japokuwa gharama ilikuwa kubwa lakini niliweza kujitutumua mwenyewe bila kuomba mchango kwa mtu yoyote.....Alisema H baba na kuongeza:
“Jambo kubwa ninalotamani litokee na ninaamini litafanikiwa ni kufunga ndoa na Flora wangu. Ninampenda sana na nina uhakika na uchaguzi wangu.”H-BABA
Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Baby Madaha, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Hisani Muya ‘Tino’, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Husna Idi ‘Sajenti’ na Wilson Makubi aliye Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania
No comments:
Post a Comment