Kiungo Maroune Fellaini wa klabu ya
Everton anatarajiwa kurudi katika mazoezi siku ya Jumatatu kwa ajili ya
kuangaliwa upya majeruhi ya goti.
Itakumbukwa
kwamba nyota huyo alipata majeruhi hayo mwishoni mwa juma katika mechi dhidi ya
Wigan waliyomaliza kwa sare ya 2-2, katika Ligi kuu ya England.
Mbelgiji
huyo ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji katika kuwania
kufuzu Michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil dhidi ya Serbia na
Scotland.
Chama cha
Soka nchini Ubelgiji kimesema Fellaini atawasili siku ya Jumatatu nchini
England katika klabu yake ya Everton kwa ajili ya kuangaliwa upya.
Taarifa ya
Klabu ya Everton imesema atakapowasili juma lijalo atafanyiwa uchunguzi kwa
mara nyingine tena pale Finch Farm.
No comments:
Post a Comment