Klabu ya Borrusia Dortmund itakosa
huduma ya kiungo wake Jakub Blaszczykowski
katika Klabu bingwa barani Ulaya juma lijalo dhidi ya Real Madrid baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mechi
ya mwishoni mwa juma nchini Ujerumani.
Taarifa ya
mtandao wa klabu hiyo imesema itakosa huduma ya kiungo huyo kufuatia mechi
waliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Hannover 96.
Pia imesema
atakosa mechi ya Poland kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil jumanne
itakayofuata.
You might also like:
No comments:
Post a Comment