• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Saturday, September 15, 2012

    TANZANIA SOCIAL NEWS: SHULE ZA KATA KUWA VYUO VYA UFUNDI


    KATIKA kukabiliana na tatizo la ajira nchini, baadhi ya wananchi wa Kata mbalimbali za wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, wamependekeza mfumo wa elimu urekebishwe na kufuta baadhi ya Shule za Sekondari za Kata na kuzifanya kuwa Vyuo vya Ufundi Stadi.
    Wananchi hao walikuwa wakitoa maoni kuhusu Katiba mpya katika Kata za Tingi, Kingerikiti, Chiwanda na Mtipwili. Mikutano hiyo inaratibiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Mkazi wa Kata ya Tingi, Maserius Mtega, alipendekeza shule za Kata za sekondari hasa vijijini zifutwe na badala yake zifanywe vyuo vya ufundi ili kuwezesha vijana wengi kupata elimu ya kujiajiri tofauti na ilivyo sasa. Alisema hali ya wanafunzi kufeli katika shule za Kata hivi sasa inachangiwa na sababu nyingi ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia, maabara na walimu hivyo kupendekeza shule hizo zigeuzwe kuwa vyuo. Akifafanua zaidi alisema imekuwa vigumu kwa serikali kuhakikisha shule hizo zinakidhi vigezo na viwango vya ubora wa elimu wakati baadhi ya wanafunzi wanaendelea kufundishwa katika hali hiyo hiyo, jambo ambalo baadae wanalaumiwa wanafunzi wakati si kosa lao. Naye Zacharia Mbunda (22) wa Kata ya Mtipwili alipendekeza shule za Kata zifutwe kwa kuwa hazina ubora
    wa kuitwa sekondari na zinadhalilisha na kushusha elimu nchini. Kwa upande wake, John Mbilinyi (19), mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kingerikiti, Kata ya Kingerikiti alipendekeza Katiba iweke mfumo bora wa elimu na kuzuia shule isiyokuwa na vigezo vya kuitwa shule, kusajiliwa. Orasto Mapunda (18), pia mwanafunzi wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kingerikiti, Kata ya Kingerikiti, alipendekeza Katiba mpya itekeleze madai ya walimu na kusimamia ubora wa elimu nchini.  Alisema Katiba iweke kipengele cha kuzuia shule kusajiliwa ikiwa haina vigezo vya ubora unaotakiwa, zikiwemo Shule za Kata alizodai wanafunzi wengi wanafeli kwa uzembe unaotokana na ukosefu wa vifaa.
    CHANZO: HABARILEO

    No comments:

    3500K