MWANAFUNZI wa darasa la nne katika
Shule ya Msingi Nyarigamba iliyoko Kata ya Muhutwe wilayani Muleba, mkoani
Kagera, Beatha James (12), ameuawa kikatili na kisha
kunyofolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili na kung’olewa meno.
Mwili
wa marehemu ambao ulipatikana baada ya siku nane maeneo ya kambi ya Jeshi la
Wananchi Kaboya, ulikutwa umechunwa ngozi, shingo imekatwa, ulimi umetolewa,
meno yameng’olewa, sehemu zake za siri zikiwa zimeondolewa na kunyolewa nywele
huku akiwa na matundu kichwani. Kwa mujibu wa maelezo ya mama mkubwa wa
marehemu, Eyudosia Salvatory, aliyekuwa akiishi naye katika Kitongoji cha
Bitende, mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani Agosti 29 mwaka huu majira ya saa
3.30 asubuhi akielekea kwa mama yake mdogo mwingine aitwaye Mariagoleti
Ishengoma.Eyudosia amesema baada ya kufika huko alitumwa akafuate
maziwa kwa jirani yao aitwaye Erasmo Sostenes, lakini akatumia muda mrefu
bila kurejea ndipo walipopiga simu sehemu wanayochukua maziwa
wakaambiwa kuwa hajafika na maziwa bado hayajachukuliwa. Na kuongeza kwamba Septemba
7 mwaka huu, ndipo walipopata taarifa za kupatikana maiti ya mtoto huyo katika
maeneo ya Kaboya karibu na kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Taarifa
za mwili huo zilitolewa na wawindaji wanaowinda wanyama waharibifu na kuwa
walipofika walikuta mwili wa Beatha ukiwa umechunwa ngozi, shingo
imekatwa, ulimi umetolewa, meno yameng’olewa, sehemu zake za siri zikiwa
zimeondolewa na kunyofolewa nywele huku akiwa na matundu kichwani, huku sura
ilikuwa imeharibika hivyo waliweza kumtambua kutokana na mavazi aliyokuwa
amevaa kabla ya kukutwa na mauti. Mtendaji wa kijiji hicho,
Dominic Damasenyi, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa
zilitolewa kwake na wanafamilia.
No comments:
Post a Comment