WAANDISHI na Wanachi mkoani Mbeya
wamelaani vikali Mauaji ya Mwandishi wa habari wa Iringa Daudi Mwangosi, aliyeuwawa Janai katika vurugu zilizotokea
katika kijiji cha Nyororo mkoani humo.
Marehemu
Mwangosi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Klabu yawaandishi wa habari mkoa wa
Iringa pia alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Chanel Ten aliuawa wakati
akiripoti vurugu zilizotokea kijijini hapo baina ya Chadema na Polisi ambapo inasemekana
alilipuliwa na bomu la machozi. Aidha kutokana na mauaji hayo waandishi na
wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari
ya Mbeya chini ya Mwenyekiti wake Christopher Nyenyembe, kwa pamoja
wamekubaliana kutoandika habari zozote zinazohusu jeshi la polisi kwa kipindi
kisichojulikana. Pamoja na tamko hilo la kutojihusisha na kazi yoyote inayohusu
jeshi hilo pia imeamriwa Jeshi hilo kutoa taarifa stahili juu ya hatua gani
walizowachukulia wahusika wa mauaji hayo ambapo pia Viongozi waandamizi
wametakiwa kujiuzulu haraka iwezekanavyo. Viongozi waandamizi waliotajwa
kujuizulu ni pamoja na Mkuu wa Jeshi hilo IGP Mwema ,Kamanda wa polisi Mkoa wa
Iringa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi kwa kile kilichodaiwa kuendelea
kufumbia macho mauaji ambayo yanaendelea kutokea katika maeneo mbalimbali
ambayo yanahusisha jeshi hilo. Pia katika maoni yao wanahabari mkoani hapa
wamevitaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ambapo imependekezwa
kutohusishwa kwa jeshi la polisi kutokana na kuhusishwa na mauaji hayo. Baadhi
ya wajumbe waliotoa maoni yao katika Mkutano wa Dharura uliofanyika katika
ofisi za Chama cha wandishi wa habari zilizopo katika mtaa wa Bhojani Katikati
ya Jiji la Mbeya wamelaani kitendo hicho ambapo wamesema jeshi hilo limeshindwa
kutambua kuwa mafanikio ya ulinzi shirikishi na polisi jamii yametokana na
ushiriki mzuri wa wanahabari. Wamesema kuwa kutokana na Jeshi hilo kushindwa
kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kufanikisha shughuli zao ni bora waandishi wote nchi nzima wakaungana ili
kulaani vitendo vya jeshi hilo na mauaji ya Mwangoka. Hata hivyo baadhi ya
wananchi wamewataka wanahabari kutokata tamaa
na kuzidi kusonga mbele bali wachukulie ni ushindi wa wanahabari na
wananchi wote kufuatia kifo cha Mwangosi hivyo ili kumuenzi ni lazima kila
mwanahabari akafanya kazi kwa bidii.
No comments:
Post a Comment