NA JAIZMELALEO
KATIKA hali ya kushangaza na
kusikitisha kuhusu usalama wa wananchi wa Tanzania hususani mkoani Mbeya, Raia
wa nchini Kenya Joseph Mbugwa ameingia nchini kinyemela na kufanya mikutano ya
hadhara bila kibali cha Polisi wala mamlaka yeyote ya kiserikali.
Hali hiyo
imebainika baada ya muda wa wiki tatu sasa raia huyo kuendelea kufanya mikutano
yake mahala mbalimbali katika Jiji la Mbeya na nje ya Jiji huku viongozi
wanaosimamia masuala ya usalama wakiwa hawajui Raia huyo kama ana kibali cha
kuingia nchini na kufanya kazi au la. Chanzo chetu kimezungumza na raia huyo
eneo la Mwanjelwa leo asubuhi ambapo amekiri kuwa hana kibali cha kufanya kazi
nchini Tanzania. Duru za kiusalama zimeeleza kuwa hata Kamanda wa Polisi wa
mkoa Diwani Athumani na wasaidizi wake nao hawana taarifa ya mikutano
inayoendelea kwa kuhamakuhama inayofanywa na Mkenya huyo. Hata hivyi imebainika
kuwa katika mikutano yake anauza kanda na CD mbalimbali ambazo anadai kuwa zina
makala za kifreemasons.
Chanzo chetu
kimeshuhudia jinsi ambavyo Mhubiri huyo kutoka nchini Kenya akiwataja wakuu wa
idara mbalimbali hapa nchini kuhusu na matukio mabaya ambayo ameyaita kuwa ya
utoaji kafara.
No comments:
Post a Comment