Wema, alifafanua kuwa anatamani kuitwa mama kwani mbali na hilo pia umri wake unazidi kusogea. Alidai kuwa ndani ya mwaka 2013 anatarajia akamilishe ishu hiyo kwani wapo baadhi ya rafiki zake ambao wana watoto na anajisikia aibu pale anapokutana nao wakiwa na watoto wao.
“Sina tatizo juu ya hilo, sasa ninaweka wazi kuwa nahitaji kuwa na mtoto lakini na katika kukamilisha malengo nataka kumpatia mtoto Diamond ingawa tulishawahi kuwa matatizo ya siku za nyuma baadhi ya watu wakadai kuwa nimetoa mimba,”. alisema Wema
Mwandishi wa DarTalk, alipomuliza Wema kuwa endapo akiwa na mtoto vipi suala zima la kula bata na kujiachia, alijibu kwa mkato kuwa hilo litaendelea lakini mwanaye atamlea kama alivyolelewa yeye na mama yake.
No comments:
Post a Comment