Ndege za kijeshi zisizo na rubani za
Marekani zimetekeleza shambulio nchini Yemen na kuua watu wasiopungua 13.
Hayo
yamethibitishwa na kingozi mmoja wa ngazi za juu wa Yemen ambaye hakutaka jina
lake litajwe na kuongeza kuwa, shambulio hilo lililofanywa na ndege za
Marekani zisizo na rubani, lilifanyika hapo jana dhidi ya watu wanaodhaniwa
kuwa na mahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida. Amesema kuwa, shambulio
hilo halikuweza kupiga eneo husika na badala yake lililenga magari mawili ya
raia katika mji wa Radda unaopatikana katika mkoa wa Al Bayda ambapo watu 13
waliuawa papo hapo wakiwemo wanawake wawili na wengine wakijeruhiwa vibaya. Wananchi
wa Yemen wamekuwa wakipinga vikali uingiliaji wa Marekani nchi mwao sambamba na
kufanya maandamano makubwa huku wakitoa nara za "Mauti kwa Marekani, Mauti
kwa Israel." Mbali na Wayemeni hao kupinga uingiliaji wa Marekani nchini
kwao, wanapinga na kulaani mashambulizi ya ndege hizo zisizo na Rubani nchini
humo ambayo mwezi uliopita yaliua idadi kubwa ya raia wasio na hatia. Hivi
karibuni Rais Barack Obama wa Marekani alijigamba akidai kuwa, kila Mmarekani
anaona fakhari kwamba nchini yake ina nguvu na inaheshimiwa kwa kuendesha
vitani zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment