Mwanamitindo na mrembo wa Tanzania aishie nchini Marekani, Teddy Kalonga Haight kwa mara ya kwanza tangu aende nchini humo, ameonekana kwenye tangazo kubwa la barabarani (billboard).
Kwa mujibu wa rafiki yake wa jimboni Texas, tangazo hilo limeonekana kwenye barabara ya mjini Houston.
“A friend of mine in Texas said she saw my billboard in Houston freeway! How excited is that! My 1st billboard in America,” alitweet jana usiku.
Kwakuwa hilo si jambo rahisi kufikiwa na model aliyehamia nchini Marekani kutoka Africa, specifically Tanzania, watu wengine maarufu waliomo kwenye industry ya modeling wamempongeza mrembo huyo.
Flaviana Matata ambaye naye hivi karibuni billboard yake ilionekana nchini Uingereza amesema: “Congrats mamiii, I know the feeling.Let’s pray for more.”
“You were born to be a star love! There will be many more of those! Keep it up,” alipongezwa na mrembo Irene Kiwia.
Miss Tanzania wa zamani Jackline Ntuyabaliwe aka Klyinn naye alimpongeza kwa kumwambia, “congratulations!that’s a good start!”
Pamoja na kuonekana kwenye Billboard hiyo, njia ya Teddy kwenye mkondo mkuu wa modeling nchini Marekani imeendelea kufunguka zaidi kwa kutumika kwa picha yake na mwanae kwenye mtandao wa Blue Cross Blue Shield of Illinois (http://www.bcbsil.com).
Pia hivi karibuni alionekana kama ‘anonymous model’ kwenye episode ya series ya ‘How Do I Look’.
“Am watchin How Do I Look and spotted Teddy Kalonga …Proudly MTZ,” alitweet mmoja wa rafiki zake.
Hongera TK!
No comments:
Post a Comment