• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, July 12, 2012

    NMB YAENDESHA DROO YA KWANZA KATIKA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB




    NMB kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea yakiwa  ni kujenga nyumba,kusomesha watoto na  kufikia malengo mengine  muhimu maishani mwao,  ilizindua promosheni inayowezesha wateja wa NMB Bonus Account an NMB Junior Account kuingia kwenye droo ya kushinda tani ya saruji,mabati ya kuwezeka,amana maradufu,ada za shule,fulana za NMB pamoja na mabegi ya shule kupitia promosheni ya Jenga maisha yako na NMB.
    Hivyo basi, leo droo ya Jenga maisha yako na NMB imechezeshwa na washindi zaidi ya 167 wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tani za seruji na mabati ya kuwezekea.
    Katika picha juu ni Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akifafanua jambo wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia na Mkuguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Sadiki Elimsu.
    Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mawasiliani wa NMB,Josephine Kulwa alisema “NMB inaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia wateja watakaoshinda kufikia malengo waliojiwekea na pia kuboresha maisha yao”
    Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akibonyeza kitufe kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB. Katikati ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, sadiki Elimsu na Meneja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia.
    Wateja wote watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye NMB Bonus Account au NMB Junior Account watapata riba ya kuvutia ambayo inaweza kuwa hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana zilizowekwa.
    Zawadi zilizoshindaniwa kwenye droo ya leo
    Zawadi
    Namba ya washindi
    Tani ya saruji (simenti)
    8
    Mabati
    3
    Double your account
    3
    Mabegi ya shule
    100
    Ada zashule
    3
    Tisheti za NMB
    150

    No comments:

    3500K