Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, inakamilisha maandalizi ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi
ambayo itafanyika tarehe 26 Agosti, 2012. Ili kufanikisha Sensa hii,
Serikali inatangaza nafasi za kazi za muda za MAKARANI NA MAKARANI
WAANDAMIZI WA SENSA kwa Watanzania wenye nia na sifa zinazostahili kama
ilivyoainishwa katika tangazo hili. Kazi hii itaanza tarehe 06 Agosti,
2012 na kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.
1. KARANI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo
atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na
atakuwa na kazi zifuatazo:-
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu;
b) Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso
fupi katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu
anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu;
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama; na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema;
b) Awe amehitimu angalau kidato cha nne;
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu,
Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi
(Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
2. KARANI MWANDAMIZI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo
atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na
atakuwa na kazi zifuatazo:- 2
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu,
b) Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso
refu katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu
anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu,
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama, na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema,
b) Awe amehitimu angalau kidato cha sita,
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu,
Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi
(Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
3. Namna ya Kutuma Maombi
Mtanzania mwenye sifa zilizotajwa hapo
juu atume maombi yake kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya
Wilaya/Halmashauri kwa anuani iliyowekwa hapa chini, akiambatisha nakala
za vyeti na nyaraka muhimu ili kuonyesha sifa alizonazo.
Maombi hayo yatumwe kwa kujaza Fomu
Maalum ya maombi ya kazi ambayo inapatikana katika Ofisi ya Mratibu wa
Sensa wa Wilaya/Halmashauri, na endapo fomu haikupatikana, mwombaji
atume maombi kwa kuandika barua akionyesha anuani kamili ya mahali
anapofanyia kazi na namba ya simu kama anayo.
Maombi yapitishwe kwa wakuu wa kazi kwa
walioajiriwa au Watendaji wa Mtaa/Kijiji kwa wale wasiokuwa na ajira,
ili maombi hayo yafike wilayani kabla ya tarehe 25 Julai, 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya
Wilaya ya ………………………..
S.L.P……………………………….……
Bofya maandishi yafuatayo kupakua:
No comments:
Post a Comment