ELCT/KARAGWE DIOCESE
Kwa wadau wote wa Maendeleo
Mkoa wa Kagera
Yah: MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE
- NYAKAHANGA DDH
Somo hapo juu linahusika.
Hospitali tajwa inaadhimisha miaka
100 tangu kuanza kutoa huduma za tiba na afya katika wilaya ya
Karagwe. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: Shabaha Yetu ni Huduma Bora
za Afya na Tiba
Maadhimisho hayo yatafanyika tangu
tarehe 27 Agosti na kilele kuwa tarehe 2 Septemba. Katika wiki hii, kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali kutakuwa na maonyesho yatakayoenda
sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi watakotembelea
mabanda yaliyoandaliwa.
No comments:
Post a Comment