Ni
mzaliwa wa Burundi lakini alihamia England kama mkimbizi yeye na
familia yake kukimbia vita nchini mwao, na sasa anatumikia uraia wa
Rwanda na anaichezea timu ya taifa ya nchi hiyo. Kwa jina anaitwa Gael
Bigirimana aliyenyoa kijogoo ambaye alikuwa akiichezea klabu ya daraja
la kwanza England inayofahamika kama New Coventry city ambapo alikuwa
akiteremsha mvua ya magoli kwenye lango la wapinzani, Lakini kwa sasa
mchezaji huyu anaweka historia kwenye
nchi za A.Mashariki kwa kuwa mchezaji pekee anayecheza ligi kuu ya
England baada ya kusajiliwa na timu ya Newcastle kwenye msimu ujao wa
ligi kuu na sasa wapinzani wategemee mvua ya magoli kutoka kwa kijana
huyu mwenye umri wa miaka 18 anayechezea nafasi ya kiungo na
mshambuliaji.HABARI ZAIDI
No comments:
Post a Comment