Siku moja baada ya Dogo Janja
kudaiwa kufukuzwa Tip Top Connection, ukweli halisi kuhusiana na uamuzi
huo umewekwa wazi na yeye mwenyewe.Sababu zilizotajwa na Tip Top
Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.
Kwa mujibu wa interview (ya pili
kufanyiwa baada ya kipindi cha Amplifaya cha jana) tuliyofanya naye kwa
simu saa moja asubuhi leo (June 14) akiwa stand kurejea nyumbani, uonevu
na dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi Dar es Salaam.
Anasema tangu aje Dar es Salaam
hajawahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku
kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye
Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.
Anasema kutokana na ngoma zake
kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa
halipwi chini ya milioni moja.Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni
kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa
tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.
“Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” ameongea uchungu.
Dogo anasema ilikuwa inafikia
wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo
na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa.Tamaa ilizidi kumwingia Madee
kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila
kujua password aliipata wapi.
“Kuna wakati nilikuwa nataka
kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina
hela sana,” anasema.Mpaka tunaongea naye asubuhi hii, anasema kadi yake
imebakiwa na shilingi 25,000 tu.
Ameendelea kudai kuwa juzi Madee
alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya
CCM na atamlipa shilingi laki moja.
“Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?”. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.
Baada
ya show kumalizika anasema yeye na back up artist wake walirudishwa saa
saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba
ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia.
Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma
sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati
hata show kumtumia kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba
yake.
“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.”
Ameendelea
kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza
alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza
kumpiga. Alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia
meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka
kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.”
Anasema simu yake alipewa jana.
Kitendo cha kumwambia Madee kuwa
amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo
hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena
kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili
wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.
“Wanajua nikiongea wataabika sana.”
Source Daily entertainment Blog
NEWS SOURCE::thisdayumagazine!
No comments:
Post a Comment