Mchezaji wa Tanzania Adam Nditi jana amesaini mkataba ‘rasmi’ kama mchezaji wa kulipwa wa klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza.
Kupitia Twitter jana ameandika; “Leo ni siku muhimu na ya kukumbuka kwangu na familia yangu na ningependa kumshukuru Mungu kwa kila kitu nilichonacho na vile navyokuwa.”
“Kuna wakati nakumbuka nilichoka kimwili na kiakili lakini baada masaa kadhaa ya mazoezi , kujituma na kufanya kazi kwa biddi naweza kusema hatimaye ndoto yangu imetimia.”
“I'd like to say well done to @Anditi3 for signing his pro contract with chelsea today! Official chelsea player! Well done bro! #cfc” alipongezwa na miongoni mwa wachezaji aliokuwa nao Chelsea Academy aitwaye Dom Solanke.
”My bro @Anditi3 signed his professional contract with Chelsea FC, well done man.” aliandika mwingine.
"Thanks again everyone for saying all the good luck and only God knows what's ahead waiting for me," Nditi alitweet.
Adam alijiunga na Chelsea Academy mwaka 2008.
Alicheza kwa mara ya kwanza msimu wa 2010-11 dhidi ya Tottenham Hotspur.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya vijana ya Chelsea iliyoshinda kombe la FA mwaka 2011-12 na mara zote alikuwa akiingia kipindi cha kwanza isipokuwa kwenye mechi ya fainali dhidi ya Blackburn Rovers, ambapo aliingia kipindi cha pili.
Adam Nditi alizaliwa tarehe 18 September 1994 mjini Zanzibar
No comments:
Post a Comment