Jeshi la Polisi mkoani
Mbeya linawashikilia watu wawili kwa
kosa la kukutwa na bangi gramu 15, tukio lililotokea Juni 7 mwaka huu majira ya
saa 12:55 jioni eneo la Machinjioni,Wilaya ya Rungwe.
Kamanda Diwani amewataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Damas
David(31) na Lusekelo Mwakalomba,ambapo hujihusisha na uuzaji na matumizi ya
bangi hizo na wote wapo mahabusu.
Aidha majira ya saa 10:45 jioni siku hiyo hiyo maeneo ya Katumba
wilayani humo; Polisi walimkamata Bi.Sophia Luvanda(40) pamoja na wenzake 14
wakiwa na pombe ya moshi(Gongo) lita 4 na mtambo mmoja wa kutengeneza pombe
hiyo.
Watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa pombe haramu ya Gongo na
mpaka sasa wote wapo mahabusu wakati upelelezi ukiendelea kuhusiana na tukio hilo na mara baada ya
upelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayowakabili.
No comments:
Post a Comment