Ilikuwa
kama muvi vile ndugu hawa walipoanza kusimulia kupitia clouds media
jinsi ya wao walivyojiunga na mlengwa wa kushoto wa maisha kama watu
wanavyodai hapa tukizungumzia Kuabudu freemason kwenye maisha yao.
Kwenye maelezo yao hawa jamaa inaonekana kabisa hawakujipanga kutoa
taarifa zilizo rasmi kwani walikuwa wakikinzana kwenye kutoa maelezo
waliyodhamiria kuyatoa ambapo walikuwa wakieleza jinsi mlengwa huo
unavyofanya kazi na wao wakiwa kama wafuasi wa mlengwa huo ambapo
walitinga studioni mwa Clouds media wakiwa na laptop yao iliyoonesha
baadhi ya mambo. Lakini wakati wa mahojiano na Zamaradi Mketema walieleza kuwa mwanachama wa mlengwa huo
ni wa dini yeyote aidha awe Muislamu au Mkristo na ndipo lilipokuja
swali kwamba "Basi mwanachama wa mlengwa huo na kundi lake hawana
ibada?" wakajibu huwezi kuwa Mromani kama hufanyi ibada za Kiromani!
Hivyo freemason lazima aje kwa ibada na kushindwa kueleza hasa mlengwa
huo unavyofanya kazi zake,!! Picha ni za jamaa hao wakiwa wanahojiwa
wakati wa kipindi cha leo tena cha Dinna
Friday, June 8, 2012
Home
Unlabelled
VIJANA WALIOJITAMBIJULISHA LEO CLOUDS FM/TV KUWA NI FREEMASON HAWA HAPA!!
No comments:
Post a Comment