T
|
aifa
Stars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa
hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania
nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.
Stars yenye kikosi cha wachezaji 20
chini ya Kocha Mkuu
Kim Poulsen
imefikia Hotel
2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa
Taifa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa
za hapa ambapo Tanzania
itakuwa saa 10 kamili.
Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim,
timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili
ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili
hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha
asicheze mechi ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment