aada ya siku chache zilizopita website hii ilikuwa ya kwanza
kuripoti kwamba klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kumsaini Marcio
Maximo, leo hii imefahamika kwamba kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa 'Taifa
Stars' Mbrazil, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena
toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9
alasiri.
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba
ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa
awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea
mwishoni.
Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa
rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika
la ndege ya Emirates.
Wednesday, June 13, 2012
Home
Unlabelled
TANZANIA FOOTBALL NEWS: MAXIMO KUTUA JUMAPILI
No comments:
Post a Comment