Mwenyekiti
wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage akionyesha waandishi wa habari
picha inayomuonyesha beki wao Kelvin Yondan akisaini mkataba wa
kuichezea Yanga jana, ambapo Simba imedai Yanga inajisumbua kwani Yondan
ni mali yao.
Rage akionyesha mkataba wa Yondan aliousaini Simba Desemba 23,2011
Simba
Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja
taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patric Yondani
kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana
wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya
Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young
Africans.
Kwamba
katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru bwana Seif
Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na klabu ya
Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya Young
imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya hilo
picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo
linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha,
pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia
benki.
Mbali
ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya mazoezi ya
timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonyesha
mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka haraka tukio hilo
limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za
ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe 6/6/2012.
Simba
Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu klabu ya Young
kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati ya Young
Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu zote za
usajili.
Kwamba
Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili na
inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na
kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka
2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari
kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
Kelvin
Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba hadi 31 mei
2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza mkataba wa awali
uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho
wa wachezaji ziko wazi katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2
kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati
mmoja.
Imetolewa leo tarehe 7/6/2012.
MH. ISMAIL ADEN RAGE (MB)
MWENYEKITI
SIMBA SPORTS CLUB

No comments:
Post a Comment