Nimepitia Blog ya http://leotainment.blogspot.com/ na kukuta hizi habari
za Wimbo Wa Ameen wa mwana FA kuwa Umeigilizia wimbo wa Cecile hey
..nimeshtuka sana baada ya kusikiliza hizo nyimbo mbili na kuona beat na
korasi zinafanana nikaamua nishare na ninyi hii habari ..sikiliza hizo
nyimbo mbili na utupie comment yako...
"Linapokuja suala la
kusample wimbo haijalishi kama msanii ni mkubwa ama mdogo watu watasema
na ukweli lazima utawekwa wazi. Kwa dunia hii ya leo yenye maendeleo
makubwa ya internet ukisample huwezi kujificha na hata ukifanikiwa ipo
siku wajanja watagundua tu.
Solothang ndiye aliyeligundua hili na
sisi tukaamua kuhakikisha na kukuta kweli Ameen ya MwanaFA ni sample ya
wimbo wa Cecile uitwao Hey aliomshirikisha Agent Sasco. Wimbo huu upo
kwenye albam yake ya mwaka jana iitwayo Jamaicanization.
Producer
wa wimbo huu ambaye ni Dully Sykes amesample wimbo huo kila kitu.
Chorus yake mwenyewe Dully ni copy and paste ya chorus ya Cecile. Kipya
kwenye Ameen iliyosifiwa sana wiki hii kwa maneno ya maana ya MwanaFA,
ni mashairi tu.
Siku zote sampling pamoja na kuwa si jambo baya
kihivyo huleta maana mbaya hasa kwa producer ambaye huonekana hana idea
kiasi cha kuchukua za wengine.
Sikiliza mwenyewe na useme kama Dully Sykes ameonewa!"
Tuesday, June 12, 2012
Home
Unlabelled
Mwana FA na Shutuma Za Kuigilizia Wimbo Wa Cecile Hey-Ameen
No comments:
Post a Comment