MWIGIZAJI wa ‘long time’ Bongo, William Mtitu ameweka bayana kuwa hakupenda
aina ya mbwa aliokuwa akiwamiliki ndiyo maana aliamua kumuuzia Irene Uwoya.
Akichezesha taya na Ijumaa kwenye ofisi zake zilizopo Magomeni jijini Dar,
Mtitu alisema alifikia uamuzi wa kuwauza mbwa hao baada ya kubaini hawawezi
kazi ya ulinzi.
“Mi’ nilishawishiwa na rafiki yangu kuwanunua nikidhani ni mbwa wa ulinzi
nyumbani kumbe ni mbwa koko.
“Sasa Mbwa gani kila unapotaka kwenda na yeye anakufuata, siyo mkali wala
nini ndiyo akatokea Uwoya nikamuuzia, nasikia na yeye kamuuza mmoja kwa
Ray,” alisema Mtitu.
No comments:
Post a Comment