Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
amesema kwamba Iran na China zipo katika kambi moja ya kupigania amani, usalama
na uadilifu duniani.
Ahmadinejad
amesema hayo jana alipozungumza na Spika wa Bunge la China Wu Bangguo pambizoni
mwa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Beijing. Aidha
amesifu msimamo chanya na endelevu wa China katika kutetea haki zisizoweza
kupingika za taifa la Iran katika taasisi za kimataifa hasa kadhia ya nyuklia
ya Iran na kusema kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia inaunga mkono haki za
taifa la China na itaendeleza mwenendo huo. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
sambamba na kuashiria kwamba mageuzi muhimu katika uga wa kimataifa yako njiani
amesisitiza kuwa, ushirikiano wa Tehran na Beijing unaweza kufanya mabadiliko
hayo yawe kwa manufaa ya mataifa na kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama
duniani na pia kuzuia kujipenyeza, kuingilia kati na kutumia mashinikizo wale
ambao wenye lengo la kuzuia nchi nyingine zisisonge mbele. Kwa upande wake Wu
Bangguo Spika wa Bunge la China amesema kuwa uhusiano wa Tehran na Beijing ni
mzuri na kutaka kuimarishwa zaidi ushirikiano wa pande mbili katika nyanja
zote.
Friday, June 8, 2012
Home
Unlabelled
GLOBAL POLITICAL NEWS: CHINA IRAN LAO MOJA
No comments:
Post a Comment