Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imempa ushindi msanii wa filamu za
maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, katika kesi ya kujadili upya umri
wake. Akitangaza ushindi huo jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Twalib
Fauz, ameupa ushindi upande wa utetezi uliopeleka ombi la kuujadili upya
umri wa msanii huyo na kuutupilia mbali umri wa miaka 18 alioandikisha
kituo cha polisi baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake,
Steven Kanumba.
No comments:
Post a Comment