H
apo kesho ni siku ya Mtoto wa Afrika
Mkoani Mbeya maandamano hayo yanadhimishwa
huku yakikabiliwa na changamoto lukuki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Child Support Tanzania Noel
Msuya Shawa amezitaja changamoto mbalimbali ikiwemo sintofahamu kwa jamii ya
kutetea watoto wenye ulemavu kufuatia dhana kuwa mtoto mlemavu hawezi chochote;
hali inayosababisha watoto hao kutengwa.
Pia
Noel Msuya ameongeza kusema katika shule za msingi na sekondari kumekuwa na
ukosefu wa vifaa vya watoto wenye ulemavu hali inayosababisha kusoma katika
mazingira magumu.
Juni
15 mwaka huu kutakuwa na maandamano ya hiari kuanzia kituo cha Stereo Kona ya
Kihumbe hadi Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya yakilenga kutetea haki za watoto
wenye ulemavu nchini Tanzania.
Siku
hiyo itapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo ya watoto walemavu yenye malengo
ya kuonyesha uwezo wao katika kazi na kuondoa sintofahamu miongoni mwa jamii.
Kauli
mbiu ya mwaka huu Haki za Watoto wenye Ulemavu, jukumu letu kuzilinda,
kuheshimu na kuwatimizia.
You might also like:
No comments:
Post a Comment