• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Thursday, June 14, 2012

    Dogo Janja Arudishwa kwao Arusha- Soma Sababu za Madee Kumrudisha


    Jana kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Msanii Madee wa Tip Top Connection ambae ndio alikabidhiwa na wazazi kumlea na kumsimamia Dogo Janja aliamplfy kuhusu sababu za kumrudisha Dogo Janja mikononi mwa wazazi wake baada ya kudai kumshindwa.

    Madee kasema “Dogo Janja aliekua form II Makongo High School kakataa kusoma kwa hiyo mimi siwezi kukaa nae wakati hataki kusoma, nilikua safarini Iringa na Mbeya ambapo baada ya kurudi mwalimu wake wa darasa alinipigia simu na kunipa pole kwa sababu Dogo Janja anaumwa, nikashtuka ikabidi nimpigie nikawa simpati kwenye simu.. nikaenda nyumbani kwa Tunda Man alipokuepo na alipojua nimekuja akajificha alikua anataka kunikimbia nikampiga sana vibao, kweli nilimpiga ambapo kesho yake baada ya kuamka nikamuuliza unataka kusoma au kuzurura mtaani? akajibu kwamba anataka kwenda kusoma Arusha ikabidi nimpigie baba yake palepale ambapo mzee wake alniomba nisimrudishe Arusha niendelee kukaa nae”

    Madee ameendelea kusema kwamba “nilimwacha nyumbani baada ya kuchukua simu yake ambapo nilikuta vitu vingi sana vya kishenzi shenzi kaviandika na ninavyo mpaka leo kwa ajili ya ushahidi, vimeniumiza hasa kwa mtu kama mimi ambae najua nimemtoa wapi, kaandika kuhusu uchafu mbaya na kingine kinanihusu mimi ambacho hapaswi kusema kwa mtu kama yeye, baada ya hapo msimamo wake ulikua vilevile kwamba anataka kurudi kwenda kusoma Arusha, jioni tukakaa kikao juzi na kaka yake na watu wengine na mimi nikampa baraka zote”

    Kwenye sentensi nyingine Madee amesema “kwa wiki iliyopita na wiki hii Dogo Janja alitoroka kwenda shule kwa siku tatu na hii ni mara ya pili ambapo mara ya kwanza nilimpeleka shule na kumchapa mbele ya wanafunzi wenzake, yani nilivyompeleka shule wanafunzi wenzake mpaka walikua wanamshangaa, alisingizia vitu vingi vya uongo alikua ananidanganya mimi nyumbani na siku hiyo ndio nilimkuta Ubungo Plaza alikua anaogelea na rafiki yake, walimu wake waliniambia hawajamuona shule kwa muda wa wiki moja”

    No comments:

    3500K