Jerry
Muro Mtangazaji/Mwandishi wa habari ambae alisimama kufanya kazi kwa
miezi kutokana na kesi ya kuomba rushwa, kesi ambayo baadae alitangazwa
kushinda, ametangaza kituo chake cha kazi baada ya wengi kutomuona kwa
muda TBC alikokua akifanya kazi.
Jerry
amesema anarudi kufanya kazi TBC na jumapili hii saa tatu na nusu usiku
ndio kipindi chake cha kwanza kitaanza kuonekana ambapo kitakua
kinaingia kwenye siasa, afya, Uchumi na mengine.
Kuhusu
kuendelea kutoa habari zake za kufichua maovu, Jerry amesema “ni kazi
ambayo iko kwenye damu yangu unajua watu wanaweka matuta barabarani
lengo ni kufika mbali japo utafika sehemu utapunguza spidi unaruka tuta
unakwenda, sasa hivi tutaifanya kwa ubora zaidi lakini pia sio siku zote
tu tuchunguze chunguze kuna saa nyingine inabidi utoe breki alafu
uangalie”
Kwenye
sentensi nyingine Jerry amethibitisha kwamba wakati alipokua kimya
baada ya kushinda kesi kuna vituo vingi vya TV Tanzania ambavyo vilitaka
kufanya kazi na yeye lakini alishindwa kwa sababu vituo vingi sasa hivi
vinafanya kazi kwa makundi ya kisiasa, vingine vimeegemea upande mmoja
ndio maana akaamua atumikie kwanza wananchi.
“Sio
kwamba TBC ndio mwisho wangu lakini ni sehemu ambayo naweza kukaa na
kuangalia nakwenda wapi nafanya nini sehemu gani, kila kitu lazima kiwe
na mwanzo kwa hiyo hilo kwangu ni mwanzo tu lakini kama nafasi nzuri
zitajitokeza basi zitapewa nafasi” – Jerry Muro
No comments:
Post a Comment