Hayo yamebainishwa na mtandao huu baada ya kufika katika Hospitali
ya Ifisi Jijini Mbeya,ambapo binti huyo alifikishwa hospitalini hapo na Mkuu wa
Kituo cha Polisi cha mji huo baada ya kupokea taarifa kwa wasamalia wema kuwa
mtoto huyo kafichwa ndani akiendelea kufanyiwa maombi na waumini wa Kanisa la
Uamusho wa Roho.
Kwa upande wake Binti huyo amejeruhiwa sehemu ya mikono,kiwiliwili
na mgongoni,amesema kuwa anaishi na Baba yake mkubwa Bwana Ambokile
Abrahamu,ambaye pia ni muumini wa dhehebu hilo lililoko eneo la Simike jijini
hapa.
Imeelezwa kuwa baba huyo alisema hakuna haja ya kwenda hospitalini
hivyo yeye na mkewe waliendelea kumfanyia maombi binti huyo na hali kuzidi kuwa
mbaya hali iliyopelekea mwili wake kuoza.
Muasisi wa kanisa hilo Mchungaji Nise Mwasomola alifariki Februari
12 mwaka 2010 na kanisa hilo linaongoza na kamati,ambapo Bwana Ambokile ni
mmoja wa wanakamati na kitendo chake cha kumzuia binti huyo kupeleka
hospitalini Jeshi la polisi lililazimika kuingilia kati.
Aidha binti huyo alifikishwa hospitalini hapo Juni 11 mwaka huu na
hali yake kwa sasa anaendelea vema baada ya kuanza kupatiwa matibabu.
Hata hivyo Jeshi la polisi linamshikilia Bwana Ambokile Abraham na
mkewe kwa kitendo hicho cha ukatili na ukiukaji wa haki za binadamu kwa
kisingizio cha imani ya kidini.
Kwa uapande wake msemaji wa Hospitali ya Ifisi Bwana Goodluck
Lession,amesema wanafanya kila jitihada ili binti huyo apone ingawa
alicheleweshwa sana
na kusikitishwa na kitendo kilichofanywa kwa binti huyo.
Mwenyekiti wa mtandao wa wanawake wa Jeshi la polisi Bi Mary
Gumbo,amewataka wananchi kufichua vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya
wanawake kwa watoto wanaowalea.
Kamanda wa Jeshi la polisi Diwani Athuman,amethibitisha kutokea
kwa tukio hili na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani pindi upelelezi
utakapo kamilika.
Mkoa wa Mbeya ni moja ya mikoa yenye madhehebu mengi,lakini mengi
yamekuwa hayazingatii maadili ya dini.
No comments:
Post a Comment