• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Saturday, February 11, 2017

    Mwanza: Akutwa na mzigo wa dawa za kulevya chumbani

    Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha pinchi 240 na ndonga mbili.



    Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa Ijumaa hii, imedai kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Kassim Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43, amekamatwa majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kanyerere kata ya Butimba wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza

    Taarifa hiyo imedai kuwa mtu huyo ni mfanyabiashara wa spear za magari katika mtaa huo.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa awali polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo.

    Aidha wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma za mfanyabiashara huyo, jana tarehe 09.02.2017, polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.

    Ilikuwa hivi , Askari walianza kufanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na taarifa hizo, ndipo ilipofika majira ya saa sita usiku askari walifika hadi nyumbani anapoishi mtuhumiwa na kuizingira nyumba yake yote na kumuona kupitia dirisha akiendelea kufunga madawa hayo kwenye vikete vidogo vidogo maarufu kama pichi.

    Wakati askari wanataka kuingia ndani ya nyumba mtuhumiwa alishtuka na kukimbiza mzigo huo wa madawa ya kulevya chooni ili kupoteza ushahidi. Aidha askari waliona kitendo kile kupitia dirishani na baadhi ya askari waliingia ndani na kufanikiwa kukuta pinchi 240 zikiwa chooni lakini bado hazikuwa zimetumbukia shimoni na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la choo.

    Polisi wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa watu aliokuwa akijihusisha nao katika biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

    No comments:

    3500K