• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, October 30, 2013

    FILAMU YA "FIGO" KUINGIA SOKONI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

    Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu za kitanzania ya Proin Promotions Limited inatarajia kuingiza movie yake nyingine sokoni mapema wiki hii. 
    Filamu ya "FIGO" ni filamu ya kitanzania ambayo imechezwa na waigizaji wakongwe katika tasnia ya filamu nchini na Ni filamu ambayo inasimimua,kufundisha na kuelemisha, Filamu ya Figo ni moja kati ya filamu ya Kitanzania ambayo imechezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kutengenezwa kwa hali ya juu na kampuni Mahiri ya Utengenezaji na Uuzaji wa Filamu Tanzania ya Proin Promotions Limited

    Proin Promotions ni moja ya kampuni kubwa ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu Tanzania ambayo tayari ishaingiza Sokoni Filamu Mbili ambazo zinafanya Vizuri kama vile Foolish Age, Long Time na sasa inakuletea Filamu ya FIGO ambayo imechezwa na Jennifer Kyaka ambaye anafahamika kama Odama, Irene Uwoya, Rachel Haule, Stanley Msungu na wengineo wengi.

    Filamu ya "FIGO" inatarajia kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa ambapo itapatikana katika maduka yote ya Uuzaji wa filamu na Kwa mawakala Wao Nchini Nzima.

    No comments:

    3500K