• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Wednesday, October 30, 2013

    BAADA YA NEY WA MITEGO KUKATAZWA KUVAA MLEGEZO....ASEMA BASATA WANAMTAFUTA


    Siku chache zilizopita mwana Hip Hop kutoka pande za Manzese Nay Wa Mitego alipokea barua kutoka BASATA inayomtaka kubadili aina ya mavazi anayovaa katika show zake (mlegezo/mtepesho) ambayo hayaendani na Tamaduni za kitanzania. 0051 Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea. “Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay. Aidha  katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya kufanya kwaajili ya kuboresha  maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi. “Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi  sana za kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay, hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini  maybe wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
    Source: Bongo5

    No comments:

    3500K