• Breaking News

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    It's more about music industry and social issues in and out of bongo land

    Tuesday, October 30, 2012

    Mastaa Wa kibongo Waongoza Kuchoropoa Mimba

    NEWZ>>>FILEX MMARI 





    ULIWAHI kujiuliza kwa nini wasichana wa mjini wanaojiita mastaa wanasifika kwa kuchoropoa mimba? Leo nitakujuza, ungana nami.
    Mwigizaji mkongwe amefyatuka. Simtaji kwa sababu mazungumzo yake hayakuwa rasmi lakini yalibeba jambo jipya kuhusiana na skendo hiyo inayosikika kila kukicha miongoni mwa mastaa wa kike wa Kibongo.


    Eti sasa hivi kutenda dhambi hiyo ni mtindo, life style au fasheni. Ni kwenda na wakati la sivyo utaachwa. Nimeshtuka. Kosa la jinai ni fasheni? Eti usipofanya hivyo utaonekana mshamba wa mji. Utabebeshwa mimba hadi ufungue kituo cha watoto nyumbani kwako. Inashangaza.
    Msanii huyo mkali anayeheshimika ana ushahidi wa staa mwenzake aliyemshuhudia akichoropoa mimba kienyeji.
    Ndiyo, kienyeji kabisa kwani tukio hilo lilitendeka nyumbani kwa msanii huyo, tena waziwazi bila kificho. Roho gani hiyo?
    Akaniambia hebu jaribu kujiuliza, mara utasikia msanii fulani ni mjamzito. Ukikaa siku kadhaa anaibuka na kusema kuwa mimba imechoropoka. Akibanwa sababu za kitabibu utasikia ooh sijui nilitumia dozi ya malaria au nilipata mshtuko. Hakuna hoja ya msingi ndani yake zaidi ya blaablaa.


    Yupo aliyesema iliingia bahati mbaya kwa sababu tu mwanaume aliyekuwa naye alimuonesha mapenzi ya dhati. Huyu naye ana hoja dhaifu kwa sababu inawezekana vipi kila mwanaume anayekuonesha mapenzi ya dhati ndiyo utende naye ngono zembe bila kufuata utaratibu wa ndoa?
    Yule naniliu yeye alisema anamshukuru Mungu kuchoropoka kwa mimba yake kwani angekongoroka na hakuwa tayari kunyonyesha. Angepoteza mvuto. Kama aliyajua hayo kwa nini akafanya ngono zembe?
    Yupo aliyebwatuka kuwa ya kwake ilichoropoka kwa sababu ya kipigo alichopewa na mpenzi wake hivyo akaona bora kuliko kumzalia mwanaume huyo kwani baadaye angekuwa msumari wa moto maishani mwake. Je, wakati anajiachia kwake hakumchunguza kwanza kabla ya kufanikisha ngono zembe?


    Kwa kuzingatia sababu mbalimbali zilizotolewa na wahusika, utagundua kuwa hawakuwa na hoja za msingi lakini hii ya kuonekana ni fasheni, sasa inatutoa huko na kudhani kuwa huwa wanafanya makusudi.
    Baadhi ya mastaa waliowahi kutajwa katika skendo hiyo na hawapaswi kuigwa katika jamii ni pamoja na Aunt Ezekiel, Wema Sepetu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya na wengine kibao.
    Tukubaliane kwamba mastaa wa Kibongo wasipobadilika kitabia hawana lolote la kuifundisha jamii zaidi ya kuipotosha. Madhara yake jamii itawadharau na hata kazi zao hazitakuwa na mvuto hivyo kupoteza mkate wa siku kwa kuwa wanaitegemea sanaa kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku. Tukubaliane kuwa wasipokubalika basi jamii iwasusie kazi zao ili wafyate mkia. For the love of game!

    No comments:

    3500K